Contact Us / Contáctenos / اتصل بنا / Hubungi Kami / Wasiliana nasi

Use the form on the right to contact us.

Utilice el formulario a la derecha en contacto con nosotros.

استخدام النموذج على الحق في الاتصال بنا.

Gunakan form di sebelah kanan untuk menghubungi kami.

Kutumia fomu ya haki kuwasiliana nasi.

         

123 Street Avenue, City Town, 99999

(123) 555-6789

email@address.com

 

You can set your address, phone number, email and site description in the settings tab.
Link to read me page with more information.

Taarifa za sera

Taarifa za Sera za Kimaudhui

Taarifa hizi za sera za kimaudhui na zinazolenga mataifa zinachunguza masuala muhimu zinazohusiana na usalama na ulinzi wa watetezi wa haki za binadamu, huku zikitoa mapendekezo kwa waundaji sera na washikadau.

Kuimarisha usalama wa mafunzo kwa watetezi wa haki za kibinadamu walio katika hatari

Ni nini watetezi wa haki za kibinadamu wanatia thamani kuhusu mafunzo ya usalama? Je, hii iinaweza kufanywa vizuri? Je, mafunzo ya usalama yanachangia aje kulinda watetezi? Aina muhimu sana ya mafunzo si ile inayozingatia juu-chini, maarifa yakihamishwa kutoka wageni waalikwa, lakini ni yale: yanayo ongeza maarifa juu ya haki; kufanya uchambuzi wa mazingira, uchambuzi wa washikandau, na tathmini ya hatari; kutengeneza mazoea ya usimamizi wa usalama; kuongea na kushauriana; kujenga mitandao ya msaada; kutafakari juu ya matendo ya kila siku kuhusiana na usalama; na kupitisha ufahamu mbalimbali wa usalama unaojumuisha ustawi wa akili na kihisia.

English, عربى , Español, Bahasa Indonesia , Kiswahili

Ustawi, hatari, na utendaji wa haki za binadamu

Watetezi wa haki za binadamu waliomo hatarini mara nyingi huona ugumu kuzungumzia ustawi wao wa fikira na hisia, hata wanapokuwa na shauku nayo. Tamaduni za utendaji wa haki za binadamu husisitiza kujinyima, ushujaa, na mateso au kifo cha kishahidi. Kanuni hizi huwazuia watetezi kuelezea wasiwasi wao na kutafuta msaada. Tutawezaje kujihusisha na majadiliano kuhusu ustawi katika utendaji wa haki za binadamu? Tutawezaje kuimarisha mbinu za kibinafsi na kijumla za ustawi kati ya watetezi waliomo hatarini?

English, عربى , Español, Bahasa Indonesia , Kiswahili


Kupinga unyanyapaa wa watetezi wa haki za binadamu

Njia ambazo watetezi wa haki za binadamu wanaona zinaathiri nafasi yao ya kazi na usalama wao. Ukandamizaji ni njia ya kawaida ya kuwazuilia, na hutokea kwa njia tofauti – kutoka kwa wito wa simu, mashtaka yasiyo ya kweli, kueneza uongo juu ya wanaharakati na kuwekelewa mashtaka. Madhara hasi ya unyanyapaji inaweza kuwa yasiyoonekana, ya hila, na ya kudumu. Yanaweza kusababisha vitisho zaidi na mashambulizi dhidi ya watetezi na ugawanyiko wa jamii. Kupinga unyanyasaji wa watetezi wa haki za binadamu ni muhimu kwa usalama na ulinzi wao, kama vile kukuza uhalali wa kazi yao ya haki za binadamu.

English, عربى , Español, Bahasa Indonesia , Kiswahili

Familia na wapendwao katika usalama na ulinzi wa Watetezi wa haki za binadamu walio katika hali ya hatari

Familia na wapendwa ni muhimu kwa maisha ya watetezi wa haki za binadamu. Kutoka kwa majadiliano na watetezi wa haki za binadamu wa Kolombia, Meksiko, Misri, Kenya na Indonesia, sera hii fupi inazungumzia njia ngumu ambazo familia na wapendwa wanahusika katika usalama na ulinzi wa watetezi walio katika hali ya hatari.

English عربى , Español, Bahasa Indonesia , Kiswahili



Gender.jpg

Jinsia, ushirikiano, na usalama

Watetezi wa haki za binadamu wanapata hatari ambazo zinaundwa na jinsia zao, mambo mengine ya utambulisho wao, masuala ya haki za binadamu wanazotetea, na hali za kijamii na kisiasa ambapo wanafanyia kazi zao. Watetezi wengine wa wanawake wanapata viwango vya juu vya ubaguzi wa kijamii na taasisi kuliko wengine; wengine pia wanabaguliwa katika harakati za kijamii za haki za binadamu. Sera hii fupi inachunguza jinsi jinsia na ushirikiano vinavyoathiri usalama wa watetezi wa wanawake, masuala wanayokabiliana nayo, na uzoefu wao wa usalama na ulinzi.

English, عربى , Español, Bahasa Indonesia , Kiswahili

Kumbuka: Angalia pia 'Muhtasari wa Matokeo' wa kila nchi, unaotoa zaidi data za utafiti.