HABARI KWA WATETEZI
Hizi ni baadhi za habari kwa watetezi wa haki za binadamu kuhusu jinsi ambavyo wanaweza kutathmini hatari, kumudu usalama, na kupokea msaada wa ulinzi. Hizi zimetolewa na mashirika tofauti na zinapatikana kwa lugha mbalimbali.
Sehemu ya kwanza inatoa viungo kwa vitabu vya mwongozo.
Sehemu ya pili inatoa habari kwa habari zingine za ulinzi, kama ruzuku za dharura, ruzuku za kuhama kwa muda; malipo kwa kazi za haki za binadamu, mafunzo mtandaoni, na taratibu za uanazuoni.
Sehemu ya tatu inatoa viungo kwa hati muhimuzinazohusiana na ulinzi wa watetezi.
Sehemu ya kwanza: Vitabu vya Mwongozo
Vitabu hivi vya mwongozo huwasaidia watetezi kutathmini hatari na vitisho wanavyopata, kutambua mazingira yao magumu na uwezo, na kukuza mpango wa utekelezaji ili kuzuia na kukabiliana na vitisho na mashambulizi. Vinaangazia masuala mbalimbali ya usalama, yakijumuisha usalama wa kimwili, usalama wa kidijitali, na ustawi wa hisia.
Bofya kwenye picha ili kupata habari
Protection International: Kitabu Kipya cha Mwongozo kwa Watetezi wa Haki za Binadamu
Kitabu hiki cha mwongozo kinapatikana kwa Kiingereza, Kifaransa na Kispanishi.
Kitabu cha Mwongozo cha Kujitunza na Kujilinda kwa Wanawake Wanaharakati
Kitabu hiki cha mwongozo kinawasaidia wanawake wanaharakati kutafakari katika muktadha yao, kujielewa zaidi na kujitunza. Inapatikana kwa Kiingereza na Kispanishi.
Usalama Kamilifu: Kitabu cha Mwongozo
Kitabu hiki cha mwongozo kinawasaidia wawezeshaji kuendesha warsha kwa watetezi ili kuwasaidia kuongeza ufahamu wao wa usalama, kubadilisha mitazamo dhidi ya ulinzi, na kuendeleza mikakati endelevu ya usalama. Inapatikana kwa Kiingereza.
Toolkit for Latin American Women H
Kitabu cha Mwongozo cha Wanawake wa Amerika Kusini Watetezi wa Haki za Binadamu Wanaoshughulikia Masuala ya Ardhi na Mazingira
Mwongozo huu unaopatikana mtandaoni unatoa habari kuhusu ulinzi kwao watetezi waliomo hatarini. Unajumuisha mwongozo kwa mashirika yanayowalinda watetezi; zawadi; taratibu za uanazuoni; ruzuku za dharura; vitabu vya mwongozo, n.k.
Security-in-a-Box
Vitabu hivi vya mwongozo kuhusu usalama wa kidijitali vinafafanua hatari ambazo watetezi hukumbana nazo katika utumizi wa tarakilishi, simu ya rununu, mtandao, na vifaa vingine. Pia, vinaangazia usalama wa data na faragha. Vinapatikana katika lugha mbalimbali, ikijumuisha Kiingereza, Kispanishi, Kiarabu, na Kibahasa Indonesia
Sehemu ya Pili: Habari zingine za Ulinzi
Kitovu cha watetezi wa haki za binadamu katika Kituo cha Centre for Applied Human Rights
CAHR inatoa habari kadhaa kwa watetezi wa haki za binadamu waliomo hatarini, ikiwemo: masomo mtandaoni , Taratibu ya Uanazuoni wa Ulinzi; msururu wa maandishi ya utafiti ya mwanzo; miradi ya utafiti; na warsha za mara kwa mara zinazowaleta pamoja wasomi, weledi na watetezi pamoja ili kutafakari juu ya maendeleo ya mfumo wa ulinzi wa watetezi waliomo hatarini.
Sehemu ya Tatu: Hati muhimu
Azimio la Haki na Majukumu ya Watu, Makundi na Maungo ya Jamii ili Kuendeleza na Kuzilinda Haki za Binadamu na Haki za Kimsingi Zinazotambuliwa Ulimwenguni ( almaarufu Azimio la Watetezi wa Haki za Binadamu) inaelezea kanuni na haki zinazohusiana na haki ya kutetea haki za binadamu. Inapatikana katika lugha tofauti, ikijumuisha Kiingereza, Kispanishi, Kiarabu, Kibahasa Indonesia na Kiswahili.
Mwongozo wa Umoja wa Ulaya wa Kuwasaidia Watetezi wa Haki za Binadamu unatoa mwongozo kwa mabalozi ya EU kuhusu jinsi ambavyo wanaweza kuwasaidia na kuwalinda watetezi waliomo hatarini katika nchizisizo za EU. Inapatikana kwa lugha mbalimbali, ikijumuisha Kiingereza na Kispanishi
Katibu maalum wa Umoja wa Mataifa anayehusika naHali ya Watetezi wa Haki za Binadamu ana mfumo wa malalamishi wa watetezi waliomo hatarini, na yeye huripoti mara kwa mara kwa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa na Baraza la Haki za Binadamu. Ripoti hizi zinapatikana kwa lugha mbalimbali, ikijumuisha Kiingereza, Kispanishi na Kiarabu.