KUHUSU UTAFITI HUU
Maelezo kuhusu miradi
Kuepuka Hatari, Kumudu Usalama, Kupokea Msaada
Mradi huu unalenga jinsi ambavyo watetezi wa haki za binadamu huepuka hatari, humudu usalama wao, na kupokea msaada wa usalama katika nchi tano- Kolombia, Meksiko, Kenya, Misri na Indonesia.
Tuliwahoji watetezi waliokumbana na hatari, vitisho au mashambulizi miaka mitano iliyopita. Tulitumia ufafanuzi mpana wa 'mtetezi wa haki za binadamu' jinsi ilivyotumiwa katika Azimio la Haki na Majukumu ya Watu Binafsi, Makundi na Maungo ya Jamii ili Kuendeleza na Kulinda Haki za Binadamu na Uhuru wa Kimsingi Zinazotambuliwa Ulimwenguni (almaarufu Azimio la Watetezi wa Haki za Binadamu), yaani, mtu yeyote anayeendeleza na kujitahidi katika ulinzi na kuafikiwa kwa Haki za binadamu na uhuru wa kimsingi.
Tuliwajumuisha watetezi kutoka matabaka pana na wanaolenga haki pana. Tuliazimia kuwa na nambari sawa za wanaume na wanawake tuliazimia kuwajumuisha watu wenye jinsia tofauti na maumbile yao ya kike au kiume. T uliwafikia kimakusudi watetezi ambao hujihusisha na haki za wanawake na mwelekeo wa kijinsia na haki za kitambulisho cha kijinsia, pamoja na watetezi ambao wamefanywa wahalifu kwa sababu za kazi zao za haki za binadamu.
Wengi walishiriki katika mahojiano kibinafsi au kikundi maalum na kukamilisha majibu ya utafiti. Idadi ndogo wahojiwa walimaliza kujibu maswali bila kuhudhuria mahojiano au kikundi. Mahojiano yalifanywa kwa lugha za Kiingereza, Kispanishi, Kiswahili, Kiarabu na Kibahasa Indonesia. Tulipokea ruhusa ya maadili ya utafiti wetu Juni 2015. Ukusanyaji wa data ulianza Julai 2015 na kukamilishwa mnamo Novemba 2016.
Huu ni utafiti mkubwa zaidi wa aina yake.
Timu and Watafiti
Mchunguzi mkuu:
Alice Nah
Watafiti:
Peter Cousins na Emily Schmitz (Kolombia)
Erick Monterrosas na Paola Pacheco Ruiz (Meksiko)
Sherif Azer (Misri)
Irina Ichim na Patrick Mutahi (Kenya)
Indira Fernida na Budi Hernawan (Indonesia)
Watafiti wasaidizi:
Patricia Bartley na Katrina Maliamauv
Mwezeshaji wa Kazi ya Sanaa:
Juliana Mensah
Wasaidizi Mwanafunzi
Helen McCall
Emilie Oelgaard
Mohamed Erwa Abdelhafez Babiker
Watafsiri
Gemma Sunyer
Salem Loret
Kurniati Shinta Dewi
Tariq M. Suleiman
Michoro
Wanachama wa Bodi ya Ushauri
Andrew Anderson, Mkurugenzi, Front Line Defenders
Enrique Eguren, Mtafiti Mkuu, Kituo cha Sera, Utafiti na Mafunzo, Protection International
Susi Bascon, Mkurugenzi, Peace Brigades International UK
Hassan Shire, Mkurugenzi Mtendaji, East and Horn of Africa Human Rights Defender Project
Anne-Sophie Schaeffer, Mkurugenzi wa Mipango, Euro-Mediterranean Foundation of Support to Human Rights Defenders
Claudia Samayoa, Mratibu, UDEFEGUA, Guatemala
Ruki Fernando, Mwenyekiti, Rights Now Collective for Democracy, Sri Lanka
Bahey el din Hassan, Mkurugenzi, Cairo Institute for Human Rights Studies, Misri
Paul Gready, Mkurugenzi, Center for Applied Human Rights, University of York