KARIBU
Hii ni tovuti ya miradi ya utafiti inayohusiana na usalama na ulinzi wa watetezi was haki za binadamu walio mashakani inayoendeshwa na Kituo cha Centre for Applied Human Rights, chuo cha University of York.
Mradi wa kwanza, Kuepuka Hatari, Kumudu Usalama, na Kupokea Msaada, unalenga mafunzo ya watetezi wa haki za binadamu Kolombia, Meksiko, Kenya, Misri, na Indonesia. Unachunguza mada kama aina za hatari watetezi hupitia; sababu zinazowafanya kuhisi salama au la; mifumo yao ya kumudu usalama; ada za usawa; na mitazamo ya ‘haki za binadamu’ na ‘watetezi wa haki za binadamu’ katika nchi hizi tano.
Mradi wa pili, Mitandao ya Usalama ya Mitandao ya usalama ya mashirika ya Kijamii na yasiyo ya serikali, unalenga jinsi ambavyo mitandao rasmi na zisizo rasmi za mashirika ya kijamii inavyotoa msaada wa ulinzi kwa watetezi wa haki za binadamu. Inachunguza masuala wanayokumbana nayo na jinsi ambavyo wanakumbana na changamoto zinazohusika katika kutoa msaada.
Tovuti hii ina matokeo ya utafiti na kazi za sanaa zilizotolewa kupitia miradi hii.