Makala ya Jarida
Katika ukurasa huu, tutaangazia makala ya jarida yanayotoa uchanganuzi muhimu wa maudhui makuu katika miradi hii ya utafiti.
Makala ya Jarida husika
Makala haya yanahusiana na usalama na ulinzi wa watetezi wa haki za binadamu waliomo hatarini.
Uhakiki juu ya Usalama na Ulinzi wa Watetezi wa Haki za Binadamu
Tangu Mkutano Mkuu wa Umoja wa Mataifa uasilishe Azimio la Watetezi wa Haki za Binadamu mnamo 1998, kumekuwa na juhudi nyingi ya kutambua na kulinda haki za watu, makundi na jamii ili kuendeleza na kulinda haki zao na za wengine. Baada ya muda, kumeibuka mfumo wa kimataifa wa ulinzi wenye wahusika wengi na ngazi mbalimbali, unaotokana na mfumo wa kimataifa wa haki za binadamu. Wahusika katika mfumo huu unaoendeshwa na malengo huasili mbinu ya ulinzi wa binadamu, na kusisitiza umuhimu wa kuwa na ufahamu wenye mwelekeo mbalimbali wa ‘usalama’. Katika makala haya, tunatambua mandeleo memaya kujitolea kwa taifa katika ulinzi wa watetezi, pamoja na mijadala, wasiwasi na majibizano ambayo bado yapo. Tunasisitiza umuhimu wa uhakiki wa makini wa ujenzi, utenda kazi na mabadiliko wa mfumo huu wa ulinzi pamoja na athari za kijamii na kisiasa za aina nyingi, zilizokusudiwa na zisizokusudiwa. Tunaangazia masuala matatu muhimu ambapo uandishi wa uhakiki unahitajika ili kuelewa aina ya mfumo wa ulinzi huu, kujadili michango ya waandishi katika toleo hili maalum: ufafanuzi na matumizi wa neno ‘mtetezi wa haki za binadamu’; ufanisi wa mifumo ya ulinzi; na uhusiano mgumu kati ya ukandamizaji, harakati na hatari. Kwa kuhitimisha, tunatambua sehemu muhimu ya utafiti zaidi inayohusiana na haki za watetezi wa haki za binadamu, tukisisitiza umuhimu wa ukuzaji wa nadharia na utendaji kuhusiana na ‘hatari’, ‘usalama’ na ‘ulinzi’.
Marejeo:
Karen Bennett, Danna Ingleton, Alice M. Nah & James Savage (2015) Critical perspectives on the security and protection of human rights defenders, The International Journal of Human Rights, 19:7, 883-895.
Ajenda ya Utafiti ya Ulinzi wa Watetezi wa Haki za Binadamu
Toleo hili maalum la Jarida la Utendaji wa Haki za Binadamu linatafakari juu ya ulinzi wa watetezi wa haki za binadamu. Katika makala haya tunatambua utafiti uliopo na maarifa kuhusu ulinzi wa watetezi wa haki za binadamu, kuonyesha michango ya sera na maelezo ya utendaji. Katika mkusanyiko huu, tunaangazia masuala ya kisasa na maswali kuhusu ulinzi wa watetezi wa haki za binadamu kwa minajili ya uchunguzi zaidi. Hasa, tunaonyesha sehemu nane za utafiti: utafiti na matumizi wa neno ‘mtetezi wa haki za binadamu’; mitazamo ya hatari, usalama na ulinzi; utamaduni, jinsia na utofauti (pamoja na mkazo juu ya ulinzi wa wanawake watetezi wa haki za binadamu); matumizi ya sheria na utawala katika ukandamizaji; ufanisi wa utaratibu wa ulinzi; mikakati na mbinu ya ulinzi; kukuza mazingira mazuri ya ulinzi wa haki za binadamu; na athari za teknolojia na usalama wa kidijitali kwa watetezi wa haki za binadamu. Katika sehemu ya mwisho ya makala haya, tunaonyesha umuhimu wa ushirikiano zaidi kati ya wanataaluma, weledi na watetezi wa haki za binadamu ili kuwezesha mageuzi ya kufana ya taratibu za ulinzi na utendaji. Tunatafakari juu ya ubora na changamoto za ushirikiano wa utafiti wa kutatua shida halisi, tukipendekeza jinsi mambo haya yatatekelezwa vyema.
Marejeo:
Nah, AM; Bennett, K, Ingleton, D and Savage, J (2013) 'A research agenda for the protection of human rights defenders', Journal of Human Rights Practice, 5(3), pp. 401-420.
Upatikanaji:
Makala haya yaliyochapishwa yanapatikana katika
Kiingereza, Kiarabu, Kifaransa na Kispanishi katika tovuti hii. Tafsiri ya Kiingereza inapatikana kubofya 'download' hapa chini.